| MH : SLAAAKIONGEA NA WAANDISHI |
WAKATI wananchi wakiwa bado
hawajalizika kuhusu Hatua alizochukua Rais Jakaya Kikwete, Juu ya maamuzi
ya Bunge kuhusu ufisadi wa Zaidi bilioni 306 kwenye Akaunti ya Tegeta
Escrow,kutokana na Rais Kikwete kulikejeri Bunge kwa kuyatupia mbali
mapendekezo mengi ya Bunge .
Nao Umoja wa Vyama vya vikuu vya Upinzani nchini ambavyo vinaunda Umoja wa
Kutetea Katiba ya Wananchi UKAWA vimeibuka na kumvaa Rais Jakaya Kikwete na
kusema anahusika kwa kiasi kikubwa kwenye Ufisadi huo, kwa kitendo chake cha
kumtetea Mmiliki wa wa kampuni ya Independent power limited (IPTL),
Bwana Harbnder Singh (Singasinga)
Na
Kusema Umoja huo utaanzisha Maandamano nchi nzima kupinga Ufisadi huo ambao
wanadai unalindwa na Rais Kikwete kutokana na yeye kuhusika katika Wizi huo .
Kauli hiyo ya Vyama hivyo vikuu vya Upinzani vinavyounda UKAWA umetolewa
leo Jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Umoja huo ambaye pia ni
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF Profesa Ibrahimu Lipumba wakati wa mkutano
na waandishi wa Habari uliohitishwa Mahususi ili kuzungumzia hutuba ya Rais
Kikwete kuhusu sakata hilo ambapo –
Profesa Lipumba alisema inasikitisha kuona Rais Jakaya Kikwete ameacha kulitetea
shirika la Umeme Tanesco na kuwatetea Mataperi wa IPTL ambao wameliingizia
hasara la mabilioni ya Fedha shirika hilo.
“Hutuba ya Rais kikwete imekuwa
mtetezi mkubwa wa Mmiliki wa PAP,anaacha kulitetea shirika la umma la
Tanesco,harafu anadanganya umma kwa kiasi kikubwa kusema kwamba pesa za
IPTL si za Umma hivi anashindwa hata kuelewa Ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Serikal
CAG ambayo inaonyesha wazi kwamba wamiliki hawa wamefanya utaperi wa wazi
kabisa katika umiliki wake “
“Taarifa za mauzo
ya Kampuni ya Mechmar kwenda piper link kwenda PAP ziliwasilishwa katika
taasisi mbalimbali za Serikali na bwana Singh sote tunafahamu ni kughushi
nyaraka ili akwepe Kodi na hili ni kosa,hivi Kikwete alioni hili?”alihoJi
Profesa lipumba.
Profesa lipumba alizidi kusema hata Maazimio yanayotokana na Taarifa ya CAG
yanaonyesha wazi kuwa PAP siyo mmiliki wa harali wa hisa za Kampuni ya
Mechmar lakini Rais Kikwete hakuliona hilo.
Kwa Upande wake Katibu
mkuu wa Muungano vyama hivyo wa Vya Upinzani vinavyounda UKAWA ambaye pia
naye ni Katibu mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Dokta Wilbroad
Slaa amesema Umoja umepanga kuzunguka nchi nzima ikiwemo kuandaa maandamano
kupinga kile wanachodai Rais Jakaya Kikwete amewalinda wezi wa Ufisadi huo.
Dokta Slaa aliongeza kuwa Kitendo cha Rais kikwete kuwatetea Wamiliki wa
kampuni ya IPTL ni wazi Rais Kikwete anahusiki kutokana na kuwepo kwa ushahidi
wa yeye kuhusika na Wezi huo.
“Tunajua wazi kwamba Rais kikwete kuhusika na wizi huu kwani kunamtu mmoja
anaitwa Guruma ambaye katika watu waliopewa pesa na bwana James Rugimalira jina
lake limetajwa kupokea mabilioni ya Fedha na mtu huyo mimi namfahamu sana,Bwana
Guruma anajulikana sana ni msimamizi wa Miradi ya Rais kikwete na leo kachukua
pesa za Escrow unategemea nini hapa na ndio maana anasuasua kuwachukulia hatua
wamiliki wa IPTL”Alisema Dokta Slaa.
Aidha,Dokta Slaa alisema kitendo cha Ufisadi huo kutokea na Idara ya
Usalama wa Taifa kushindwa kulinda nchi kwenye ufisadi huo ni wazi idara
hiyo imeshindwa kazi.
“Usala wa
Taifa upo kila Barozi inashangaza sana kuona Idara hii inashindwa kuona utaperi
wa mmiliki wa IPTL au tutegemee nini ndio maana hata kwenye Ufisadi wa
EPA,tuliona Jinsi Kampuni iliyokuwa ikimilikiwa na Ofisa wa Usalama wa Taifa
ilivyochota pesa unategemea nini”
“Na hata Kikwete alivyosema mara baada ya kutua uwanja wa ndege alipotoka
kutibiwa anavyosema alijui sakata hili kutokana na yeye kuwa kwenye matibabu ,
ni kuwadanganya watanzania kwani baada ya masaa mawili kutoa uwanja wa ndege
hapo,niliona email aliyekuwa akitumiana na bwana Rugimalira,sasa huyo ni
kiongozi kweli”alihoji Dokta Slaa.
Naye Mwenyekiti wa chama cha
NCCR Mageuzi James Mbatia alisema ni Rais kikwete amekosa maamuzi katika nchi
kutokana na kitendo chake cha kushindwa kuwachukulia hatua waliohusika na
kusema pesa za wananchi zimepotea huku taifa likiosa fedha hususani wao
wabunge mapaka sahivi hakuna hata mbunge aliyepata hata mshahara.
Umoja huo wa UKAWA ni muunganiko wa Vyama vya CHADEMA,CUF na NCCR pamoja NLD.
Facebook
Twitter
Google+
Rss Feed

0 comments: