Powered by Blogger.
Showing posts with label matukio. Show all posts
Showing posts with label matukio. Show all posts

Sunday, 4 January 2015

SHIDAAAH!!:: WATCH OUT RAY C AKIMBIZWA PEKUPEKU NA PANYA ROAD HADI KITUO CHA POLIS...

Posted by Unknown at 12:49 0 Comments


 

   


juzi mambo yalikuwa si mambo katikati ya jiji la dar baada ya vijana wanaojiita panya road kufanya fujo mitaa ya sinza, magomeni na mwananyamala , mmoja wa wahanga wa fujo hizi ni mwanamuziki ray c..

hichi ndicho kilichomtokea:

"sina hamu na hawa panya road, jana nilikuwa sehemu flani sinza nakula kitimoto nilivyoona watu wanakimbia nikatoka nduki bila viatu nikaingia kwenye gari mbio mara mbele yangu nikakutana na lundo la watu wakinoa mapanga barabarani, niligeuza gari utafikiri niko kwenye movie nikajikuta nimefika osterbay polisi bila viatu mpaka askari wakanicheka! !!!!!!!!!!serikali tunaomba mkamate hawa vijana kwakweli maana tumezoea amani sasa mambo kama haya yakitokea yanakosesha amani kabisa kwa wananchi!na uhakika jeshi la polisi litafanya kazi yake yani nilijihisi kama niko rwanda maana nakumbuka mapanga yale niliwahi yaona kwenye muvi ya somewhere in april na hotel rwanda!!!!sasa wale waliosema bora damu imwagike nadhani kauli itabadilika maana kama panya road wanatupelekesha hivi je hiyo vita!!!, je hiyo vita, si tutapanda juu ya nyumba zetu!!!!! jamani msicheze na haya mambo jamani, amani ndio sifa kuu ya nchi yetu........eeh mungu tuepushe na haya mambo....." ray c

Tuesday, 30 December 2014

SIKU ZA MWISHO :: TAZAMA VIDEO WANAUME WAOANA MBELE YA MAELFU YA WATU KATIKA KANISA LA ...MBELE YA BADRI MARKOS THONG

Posted by Unknown at 17:13 0 Comments
"Dunia hii itafanywa tupu kabisa, na kuharibiwa kabisa; maana BWANA amenena neno hilo. Dunia inaomboleza inazimia; ulimwengu unadhohofika unazimia; watu wakuu wa dunia wanadhoofika. Tena dunia imetiwa unajisi kwa watu wanaoikaa, kwa maana wameziasi sheria, wameibadili amri, wamelivunja agano la milele". ISAYA 24:3-5.


Mambo 3 yamezungumziwa ktk msitari wa 5 ambayo ndiyo sababu ya dunia hii kuwa ktk hali hii mbaya:

1. KUZIASI SHERIA - Hii inamaanisha ni kutenda kinyume na sheria za Mungu zinavyosema 'KUTOKA 20:3-17.

2. KUIBADILI AMRI - Hii inamaanisha kuna amri moja iliyobadilishwa maana inazungumzia uchache. Na ukiangalia leo amri ya 4 ndiyo iliyobadilishwa 'KUTOKA 20:8-11, hata Daniel naye alitabiri kuhusiana na jambo hili "DANIEL 7:25".


3. KUVUNJA AGANO LA MILELE - Agano hili la milele lilivunjwa ni Sabato ya Bwana 'KUTOKA 31:16

"Dunia hii itafanywa tupu kabisa, na kuharibiwa kabisa; maana BWANA amenena neno hilo. Dunia inaomboleza inazimia; ulimwengu unadhohofika unazimia; watu wakuu wa dunia wanadhoofika.

Tena dunia imetiwa unajisi kwa watu wanaoikaa, kwa maana wameziasi sheria, wameibadili amri, wamelivunja agano la milele". ISAYA 24:3-5. Mambo 3 yamezungumziwa ktk msitari wa 5 ambayo ndiyo sababu ya dunia hii kuwa ktk hali hii mbaya:

1. KUZIASI SHERIA - Hii inamaanisha ni kutenda kinyume na sheria za Mungu zinavyosema 'KUTOKA 20:3-17. 2.

KUIBADILI AMRI - Hii inamaanisha kuna amri moja iliyobadilishwa maana inazungumzia uchache. Na ukiangalia leo amri ya 4 ndiyo iliyobadilishwa 'KUTOKA 20:8-11, hata Daniel naye alitabiri kuhusiana na jambo hili "DANIEL 7:25". 3.

KUVUNJA AGANO LA MILELE - Agano hili la milele lilivunjwa ni Sabato ya Bwana 'KUTOKA 31:16

MAAJABU ::JIONEE PICHA AJIFUNGUA AKIWA NA UMRI WA MIAKA 5 NDIE MWANAMKE MDOGO DUNIANI KUJIFUNGUA

Posted by Unknown at 10:50 0 Comments

     Lina Medina aliyezaliwa tarehe 27 Sept. 1933, huko Ticrapo, mkoa wa Huancavelica, nchini Peru, anatajwa kua Mama mwenye umri mdogo kuwahi kutokea katika historia ya Ulimwengu.
Tarehe 14 Mei 1939 Lina akiwa na umri wa miaka 5 na miezi 7, alijifungua mtoto wa Kiume aliye mpa jina la Gerardo Medina. 

Ilianzaje? Mwanzoni mwa mwezi Machi 1939 wazazi wa Lina ~ Tiburelo Medina na Victoria Losea waliamua kumpeleka Hospitali baada ya kuona tumbo likiongezeka kupita kiasi.Wazazi wa Lina walidhani huenda ana uvimbe tumboni, lakini madaktari waligundua kua alikua ana ujauzito wa miezi 7. Dr. Gerardo Lozada aliamua kumpeleka Lina kwa wataalam zaidi nao wakathibitisha kua ni kweli alikua mja mzito. 

Alizaaje? Mwezi mmoja na nusu baada ya kupelekwa hospitali kwa mara ya kwanza, Lina alijifungua mtoto wa kiume kwa njia ya upasuaji, kutokana na njia yake ya uzazi kua ndogo. Upasuaji ulifanywa na Dr. Lozada, Dr. Busalleu, na Dr. Colareta. 

Alivunja Ungo lini? Dr. Edmundo Escomel alitoa ripoti kamili juu ya kesi ya Lina kupitia jarida maalum la maswala ya kiafya na matibabu liitwalo La Presse Médicale. Ripoti hii ilibainisha kwamba Lina alianza kupata siku zake tangu akiwa na umri wa miezi 8, alitofautiana na ripoti ya awali iliyosema kua amekua akiona siku zake tangu alipokua na umri wa miaka 3. Ripoti hii pia ilisema kua Lina alianza kuota maziwa akiwa na umri wa miaka 4, alipofikisha miaka 5 nyonga yake ilikua imesha tanuka. 

Alizaa mtoto gani? Mtoto alizaliwa na uzito wa kilo 2.7 na alipewa jina la daktari wake Gerardo.
Gerardo alilelewa akijua kwamba lina ni dada yake lakini alikuja kujua ukweli akiwa na umri wa miaka 10.
Gerardo aliendelea kukua akiwa mtoto mwenya afya njema lakini alifariki mwaka 1979 akiwa na miaka 40 kwa ugonjwa wa mifupa ujulikanao kwa jina la kitaalam la Bone marrow.

Nani Baba wa mtoto? Lina hajawahi kumtaja baba wa mwanae wala mazingira yaliyopelekea yeye kupata mimba. Dr. Escomel alipendekeza kwamba inawezekana hata Lina mwenyewe alikua hajui, na kusema kua hakutoa majibu yanayo jitosheleza. 

Tuhuma kwa baba mzazi: Hata hivyo Baba mzazi wa Lina alikamatwa na kushitakiwa kwa kosa la Unyanyasaji wa kingono wa mtoto (Child Sexual Abuse) lakini aliachiwa baadae baada ya kukosekana ushahidi wa kutosheleza. Na hivyo basi Baba halisi aliyempa mimba Lina hakuwahi kujulikana 

Maisha ya Lina baadae:
Miaka kadhaa baadae Lina aliolewa na Raúl Jurado ambaye mwaka 1972 walipata mtoto wa kiume. Lina yupo hai mapaka sasa na anaishi maisha ya kimasikini huko Lima nchini Peru

Monday, 29 December 2014

HIVI PUNDE:JIONEE PICHA NA VIDEO ABAKWA NA WANAUME ZAIDI YA 100 BAADA YA KUMBAKA MTOTO WAKE WA KIUME

Posted by Unknown at 17:32 0 Comments
Tukio la kusikitisha lilotokea hivi karibuni nchini Marekani katika Jimbo la Philadelphia la mama mmoja kumbaka mtoto wake na kuwaudhi watu na kujikuta na yeye akibakwa na wanaume 120.
Tukio hilo lilitokea majira ya jioni ambapo walisikia kelele za mtoto alikilia kama mtu aliekabwa na walimfuata walimkuta mtoto huyo akivuliwa nguo na mama ake ambapo mama ake alikuwa ameshavua nguo tayari yuko uchi wa mnyama tayari kwa kubaka.
Mama huyo alijikuta akibakwa na wanaume 120 kwa zamu bila utetezi wa watu wowote kwa sababu watu wa maeneo hayo hawakufurahishwa na kitendo chake hicho alichotaka kumfanya mtoto wake, mama huyo alionekana kama mtu mwenye pepo la ngono kwa kuwa si mara ya kwanza kufanya tukio la namna hiyo, ambapo mwazo alishawahi kufanya tukio kama hilo kabla na kupewa onyo kali asirudie tena, kwa kuonekana kwake kurudia tukio hili ndipo ghalika la kubakwa na watu 120 lililomkuta.
Tukio la hivi linatoa baadhi ya ishara za mwisho wa dunia kwani wanadamu wanaonekana kufanya matukio ya kinyama ambayo binadamu hapaswi kufanya.

Friday, 26 December 2014

HATARI YATANDA SONGEA;:JIONEE PICHA WIZI WA SANAMU YA BIKRA MARIA NA MILIPUKO YA MABOMU

Posted by Unknown at 13:24 0 Comments
Vijana watatu Songea wametakiwa kwenda na wazazi wao kutubu dhambi za kutaka kuiba sanamu la Bikira Maria katika Kanisa Katoliki la Kigango cha Samora.
Katekista wa Kigango hicho Keneth Mhagama walisema vijana hao walifanya jaribio hilo usiku wa manane baada ya ibada ya mkesha ambapo walinzi walifanikiwa kuwadhibiti kabla hawajafanikiwa na wakawekwa mbaroni.
Vijana hao ni Ahmed, Mohammed na Leonard ambapo Padri wa Kanisa hilo Cristom Kapinga amesema vijana hao wanatakiwa kutubu la sivyo watawaacha kwenye mikono ya sheria washughulikiwe.
Chanzo cha Habari: Gazeti Mtanzania

Wanasayansi wako kazini… Safari hii wametafiti hii ya wanaume kunyonyesha watoto

Posted by Unknown at 12:54 0 Comments
Dunia na maajabu yake kwenye siku nyingine, leo kuna tafiti inayosema kuwa eti wanasayansi wanasema kwa kuangalia vigezo vya kibaiolojia wanaume wanaweza kunyonyesha hivyo huenda muda mfupi ujao jukumu hilo lisiwe la wanawake peke yao.
Dr. Semkuya kutoka Hospitali ya Mwananyamala amesema mwanaume anaweza kutoa maziwa lakini sio maziwa yafaayo kwa lishe ya mtoto.
… Wapo wanaume wanaochezea chuchu kwa muda mrefu na kufanya hivi wanaweza kusababisha maziwa kutoka…Dk. Semkuya
Daktari mwingine mstaafu anasema hivi; Wanaume wana tezi zao na wanawake wana tezi za kipekee ambazo zinawasaidia kuzalisha maziwa…”— Dk. Malise Kaisi.
Daktari mwingine bingwa wa magonjwa ya binadamu Meshack Shimwela amesema mwanaume anaweza kutoa majimaji katika chuchu zake lakini hayo sio maziwa.
Iliwahi kuripotiwa kuwa mwaka 2002 kulikuwa na mwanaume aliyeamua kumnyonyesha mwanae baada ya kufiwa na mke wake Sri Lanka, lakini story ni kwamba Jarida laLancet limeeleza kuwa mwanaume anapokaa na mtoto mchanga na kuamua kunyonyesha tezi za maziwa zinazoitwa lobules huzalisha maziwa hivyo kukawezekana mwanaume kunyonyesha maziwa kama ya mwanamke.
Ripoti ya Jarida hilo imesema kwa watu wenye jinsia mbili kuna uwezekano sio wa kunyonyesha tu, bali hata kubeba ujauzito kutokana na mchanganyiko wa homoni.
Comment yako mtu wangu wa nguvu, unadhani ikithibitika hii ya wanaume kunyonyesha hali itakuwaje?
Chanzo cha Habari: Gazeti MwananchiDecember 26.

Wednesday, 24 December 2014

MTIKISIKO MKUBWA SERIKALINII ::MAMBO MAZITO YALIOADHIMIWA NA UKAWA JUU YA JK NA KUKING'OA CHAMA TAWALAFUATILIA MKASA HUU

Posted by Unknown at 13:19 0 Comments
MH : SLAAAKIONGEA NA WAANDISHI








WAKATI wananchi wakiwa bado hawajalizika kuhusu  Hatua alizochukua Rais Jakaya Kikwete, Juu ya maamuzi ya Bunge kuhusu ufisadi wa Zaidi bilioni 306 kwenye Akaunti ya Tegeta Escrow,kutokana na Rais Kikwete kulikejeri Bunge kwa kuyatupia mbali mapendekezo mengi ya Bunge .
       Nao Umoja wa Vyama vya vikuu vya Upinzani nchini ambavyo vinaunda Umoja wa Kutetea Katiba ya Wananchi UKAWA vimeibuka na kumvaa Rais Jakaya Kikwete na kusema anahusika kwa kiasi kikubwa kwenye Ufisadi huo, kwa kitendo chake cha kumtetea Mmiliki wa wa kampuni ya Independent power  limited  (IPTL), Bwana Harbnder Singh (Singasinga)
     Na Kusema Umoja huo utaanzisha Maandamano nchi nzima kupinga Ufisadi huo ambao wanadai unalindwa na Rais Kikwete kutokana na yeye kuhusika katika Wizi huo .
        Kauli hiyo ya Vyama  hivyo vikuu vya Upinzani vinavyounda UKAWA umetolewa leo  Jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Umoja huo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF Profesa Ibrahimu Lipumba wakati wa mkutano na waandishi wa Habari uliohitishwa Mahususi ili kuzungumzia hutuba ya Rais Kikwete kuhusu sakata hilo ambapo –
       Profesa Lipumba alisema inasikitisha kuona Rais Jakaya Kikwete ameacha kulitetea shirika la Umeme Tanesco na kuwatetea Mataperi wa IPTL ambao wameliingizia hasara la mabilioni ya Fedha shirika  hilo.
“Hutuba ya Rais kikwete imekuwa mtetezi mkubwa wa Mmiliki wa PAP,anaacha kulitetea shirika la umma la Tanesco,harafu anadanganya umma kwa kiasi kikubwa  kusema kwamba pesa za IPTL si za Umma hivi anashindwa hata kuelewa Ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Serikal CAG  ambayo inaonyesha wazi kwamba wamiliki hawa wamefanya utaperi wa wazi kabisa katika umiliki wake “
   “Taarifa za mauzo ya Kampuni ya Mechmar kwenda piper link kwenda PAP ziliwasilishwa katika taasisi mbalimbali za Serikali na bwana Singh sote tunafahamu ni kughushi nyaraka ili akwepe Kodi na hili ni kosa,hivi Kikwete alioni hili?”alihoJi Profesa lipumba.
        Profesa lipumba alizidi kusema hata Maazimio yanayotokana na Taarifa ya CAG yanaonyesha wazi kuwa PAP siyo mmiliki wa harali wa  hisa za Kampuni ya Mechmar lakini Rais Kikwete hakuliona hilo.



Kwa Upande wake Katibu  mkuu wa Muungano vyama hivyo wa Vya Upinzani vinavyounda UKAWA ambaye pia naye ni Katibu mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Dokta Wilbroad Slaa amesema Umoja umepanga kuzunguka nchi nzima ikiwemo kuandaa maandamano kupinga kile wanachodai Rais Jakaya Kikwete amewalinda wezi wa Ufisadi huo.
       Dokta Slaa aliongeza kuwa Kitendo cha Rais kikwete kuwatetea Wamiliki wa kampuni ya IPTL ni wazi Rais Kikwete anahusiki kutokana na kuwepo kwa ushahidi wa yeye kuhusika na Wezi huo.
     “Tunajua wazi kwamba Rais kikwete kuhusika na wizi huu kwani kunamtu mmoja anaitwa Guruma ambaye katika watu waliopewa pesa na bwana James Rugimalira jina lake limetajwa kupokea mabilioni ya Fedha na mtu huyo mimi namfahamu sana,Bwana Guruma anajulikana sana ni msimamizi wa Miradi ya Rais kikwete na leo kachukua pesa za Escrow unategemea nini hapa na ndio maana anasuasua kuwachukulia hatua wamiliki wa IPTL”Alisema Dokta Slaa.
        Aidha,Dokta Slaa alisema kitendo cha Ufisadi huo kutokea  na Idara ya Usalama wa Taifa kushindwa kulinda  nchi kwenye ufisadi huo ni wazi idara hiyo imeshindwa kazi.
    “Usala wa Taifa upo kila Barozi inashangaza sana kuona Idara hii inashindwa kuona utaperi wa mmiliki wa IPTL au tutegemee nini ndio maana hata kwenye Ufisadi wa EPA,tuliona Jinsi Kampuni iliyokuwa ikimilikiwa na Ofisa wa Usalama wa Taifa ilivyochota pesa unategemea nini”
       “Na hata Kikwete alivyosema mara baada ya kutua uwanja wa ndege  alipotoka kutibiwa anavyosema alijui sakata hili kutokana na yeye kuwa kwenye matibabu , ni kuwadanganya watanzania kwani baada ya masaa mawili kutoa uwanja wa ndege  hapo,niliona email aliyekuwa akitumiana na bwana Rugimalira,sasa huyo ni kiongozi kweli”alihoji Dokta Slaa.
 

Naye Mwenyekiti wa chama cha NCCR Mageuzi James Mbatia alisema ni Rais kikwete amekosa maamuzi katika nchi kutokana na kitendo chake cha kushindwa kuwachukulia hatua waliohusika na kusema pesa za wananchi zimepotea huku taifa likiosa fedha hususani  wao wabunge mapaka sahivi  hakuna hata  mbunge aliyepata hata mshahara.




        Umoja huo wa UKAWA ni muunganiko wa Vyama vya CHADEMA,CUF na NCCR pamoja NLD.

Total Pageviews

back to top